FAHAMU KUHUSU TEZI DUME NA JINSI YA KUONDOKANA NA TATIZO HILI.






 Elimu ya tezi dume ni pana sana na inayohitaji umakini sana kuifuatilia,
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini.
Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo.
Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili.
Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mno. Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi.

Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume.
Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume.

  Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50.

Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika na saratani ya Tezi Dume,
mtu 1 kati ya watu 6 analo hili tatizo; 3% (1 kati 33) wanakufa kwasababu ya Saratani ya Tezi Dume.
 Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.

II. VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA




Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi.
Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jamii kuhusu afya zao.

Vifuatavyo ni vyanzo vya kutanuka kwa tezi dume.
- Ukosefu wa lishe kamili na Virutubisho muhimu mwilini
- Uwepo wa sumu nyingi mwilin
- Kutokufanya mazoez
- Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara
- Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitamb
- Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance)
- Msongo wa mawazo ( Stress )
- Magonjwa ya zinaa
- Umri mkubwa
- Upasuwaji wa korodani, kuzaliwa na korodani moja,
- Historia ya Familia (Kurithi)
- Sababu za kimazingira (Ethnicity)

III. DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME

Mtu mwenye tatizo katika tezi huanza kwa dalili ndogo ndogo sana,
Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), ujue amekaa na tatizo hilo kwa muda mrefu, si chini ya miaka isiyopungua 10.
Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo (Urethra) wakati unakojoa; ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija; baada ya muda unazalisha “Uric Acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer).
Saratani ziko stage nne.
 Ya kwanza na yapili ukiwahi unaweza kupona; lakini ikishafika stage ya 3 na 4, hazitibiki bali  Unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.

Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla hujaharibu mfumo wako
mzima wa uzazi wa mwanaume.



a) Dalili za awali
- Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
- Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
- Maumivu kwenye mfumo wa mkojo
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.
- Homa
- Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku

b) Dalili za mtu aliyeathirika

- Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
- Miguu kuwa dhaifu
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa , au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
- Kushindwa kuzuia mkojo, pindi unapohisi kukojoa
- Kushindwa kuzuia haja kubwa (kinyesi cha maji maji)
- Tumbo kuja gesi mara kwa mara

IV. MADHARA YA TEZI ILIYOTANUKA

Katika hatua za awali, tezi inapotanuka hugunduliwa kwa kupimwa kwa njia ya kidole. Hii ni njia ambayo daktari huingiza kidole kwenye njia ya haja kubwa ili kuweza kubaini kama tezi imetanuka. Kipimo hiki ndicho rahisi kinacho kubalika duniani kote na kisicho na gharama.
Lakini kimekuwa kikipata upinzani kutoka kwa wanaume kutokana na imani potofu ya wahusika wa tatizo hili kuona ni udhalilishaji.


Kipimo kingine ni kipimo cha damu. Damu huchunguzwa aina ya protein inayozailishwa na seli za tezi dume, kiitwacho Prostate Antigen (PSA). PSA huonesha kuwapo kwa tatizo kwenye Tezi Dume, lakini kipimo hiki hakina uwezo wa kutofautisha endapo tatizo hilo linamaanisha saratani.

Yafuatayo ni madhara ya tezi iliyotanuka

- Kibofu cha mkojo kuuma: hivyo hupelekea mkojo kurudi juu, na kuharibu figo na Ini n.k.
- Kufunga kwa njia ya mkojo kabisa
- Figo kushindwa kufanya kazi (Kidney Failure)
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa (Ndoa zinavunjika)
- Ugumba (Infertility, Frigidity for men)
- Kutokea kwa majipu sehemu ya Tezi Dume
- Kifo


V. SULUHISHO KWA TEZI ILIYOTANUKA

a) Suluhisho Linalopendwa
Watu wengi hukimbilia hospitali pindi wanapopatwa na madhara ya Tezi dume na kujikuta wakipewa tiba ambazo huficha tatizo hilo kwa muda mfupi kisha tatizo hujirudia kwa kasi kubwa.
Tezi iliyotanuka haiwezi kutibika kwa njia za madawa yenye makemikali au mitishamba, lakini madawa au upasuaji hupunguza maumivu ya dalili na kuzifanya zisizidi sana.
Kuna njia 3 za kudhibiti Tezi iliyotanuka

1. Kusubiri na kufuatilia kwa ukaribu na Daktari:
Inashauriwa kwamba kwa tatizo hili ni bora kuendelea kulichunguza bila kukimbilia tiba kali kama madawa, upasuaji na Tiba kemikali, mpaka pale mtu atakapoona hakuna njia mbadala.
2. Madawa
Waaathirika wa tatizo la tezi dume hupewa baadhi ya madawa ili kuweza kuondoa maumivu wayapatayo.
Lakini wataalamu wengi wa afya wametokea kuyapinga sana matumizi ya madawa hayo kutokana na madhara ambayo watumiaji huyapata.
Baadhi ya madawa wanayopewa wagonjwa wa saratani ya tezi Dume yaligunduliwa miaka 30 iliyopita, yanasababisha athari kwenye Ini, Moyo na kuvimbisha magoti. Yamepigwa marufuku katika Nchi haswa za Ulaya.”
– Johnathon Waxman, Cancer Specialist, Hammer Smith Hospital, London

3. Upasuaji
Njia hii ambayo madaktari hutumia inapelekea “70% ya wagonjwa kuwa mahanithi baada ya upasuaji, na 40% wanashindwa kuzuia mkojo kutoka wanapo banwa na haja ndogo.”
– Johnathon Waxman
Inasikitisha kuona wanaume wanapasuliwa bila uhakika wowote kwamba huo upasuaji utakuwa na manufaa.


SULUHUSHO BORA.

Kama tulivyosoma vyanzo vyake tezi dume hutanuka kwasababu ya upungufu wa madini na virutubisho muhimu ambavyo mwili unavihitaji. 

Virutubisho hivyo husaidia katika kuimarisha kinga dhidi ya mwili na kuzuia ongezeko la uzalishwaji wa bacteria ambao wakizidi  hupelekea Saratani ya tezi.

Kwa  aajili ya kuondokana na changamoto hii ya kutanuka kwa Tezi Dume, na mfumo wa uzazi mwanaume.
Kampuni tumewaandalia program ya lishe kamili na virutubisho muhimu ambavyo siyo dawa wala mitishamba. 
Zimetengenezwa kwa kutumia virutubisho lishe ambavyo tungefaa kula kila siku katika vyakula vyetu, Vina lishe kamili na virutubisho muhimu kwaajili ya mwili wa mwanaume ili kutengeneza  afya bora na nadhifu.
Vina mchanganyiko wa: 
Proteins, Vitamins, Minerals, Essential Fat Acid and Trace minerals.

Virutubisho hivi
Vimeidhinishwa na taasisi mbalimbali za kimataifa na kuruhusiwa kutumiwa na mpaka sasa nchi zaidi ya 160+ hutumia virutubisho hivi.



Kwa yeyote anayehitaji hii program hii wasiliana nasi na utaipata popote ulipo Tanzania au Nje ya Tanzania.

                MAWASILIANO YETU.

HEALTHY LIFESTYLE CONSULTANTS.

                  +255654399788
                  +255763006605
                


    Happiness is nothing more than good health and a bad memory. 

                 Albert Schweitzer




Comments

  1. Casino Las Vegas (Vegas) - MapYRO
    Find the best casino in Las Vegas (Vegas) with 1087 Reviews, 156 Photos, 충주 출장마사지 and 군산 출장마사지 83 Reviews. 충청북도 출장안마 Hotel? trivago! Rating: 7.8/10 · 경상남도 출장샵 ‎2,807 reviews 거제 출장마사지 · ‎Price range: 0

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

FAHAMU KUHUSU NGUVU ZA KIUME NA JINSI YA KUONDOKANA NA TATIZO HILO.